Welcome to Coastal High School of Tanga
Shule ya Sekondari Coastal ni shule ya binafsi chini ya kampuni ya Bright & Mathew enterprises LTD iliyosajiliwa kuanzia tarehe 10/09/2000 kwa namba ya usajili S.977 kwa mujibu wa kifungu 26 cha sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978. usajili huo ulikuwa ni kwa kidato cha tano na sita pekee. Mnamo tarehe 22/8/2011 shule ilipata kibali cha kuanzisha masomo ya kidato cha kwanza hadi cha nne (1-4), namba ya kituo cha mtihani ni S.1174. Shule ya Sekondari Coastal ni ya wavulana na wasichana ikihudumia wanafunzi wa kitanzania kutoka maeneo yote ya Bara na visiwani. Wanafunzi wote wa kike na wa kiume wanapata haki sawa ya Elimu katika mazingira yetu hali inayowafanya wahitimu wote wajenge hali ya kujiamini na kufuta dhana potofu ya ubaguzi wa kijinsia. Shule ya sekondari Coastal (coastal high school), ni kwa ajili ya wanafunzi wa Kutwa na Bweni ndani ya mkoa wa Tanga na nje ya Mkoa wa Tanga. Imekuwa na historia Nzuri kwakuwa inapokea wanafunzi kutoka mikoa mbalimbali kwa uwiano mzuri wa kijinsia. vyumba vyote vya mabweni vinajitosheleza kwa huduma (self- contained room) Shule ya sekondari Coastal ilipitia maboresho makubwa mwaka 2018. Mabadiriko hayo makubwa yaligusa maeneo makuu matatu; i) taaluma ii) nidhamu na ii) usalama wa shule na wanafunzi. Shule ya Sekondari Coastal haina mfungamano na imani ya dini yoyote. Inatoa uhuru wa kuabudu kwa wanafunzi wa dini na madhehebu yote kulingana na utaratibu uliopo shuleni. Kwasababu hii, wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Coastal wanalelewa katika maadili mazuri sana hali inayopelekea kutokwepo kwa matukio makubwa ya utovu wa nidhamu. Shule ya Sekondari Coastal ina rekodi nzuri sana kitaaluma, mapinduzi makubwa katika eneo la taaluma hasa kimfumo yamepelekea shule kuwa katika namba Moja kwa wilaya ya Tanga mjini na kushika nafasi nne za juu kimkoa na 30 bora kitaifa katika mitihani ya Taifa. Kwa kidato cha sita katika mtihani wa taifa, shule imefanikiwa kufuta daraja 0,4 na 3 kwa miaka Minne mfululizo kwani shule imeboresha kiwango cha ufaulu wake hadi kufikia daraja la 1 na 2 pekee kitaifa. Jambo la kusisimua ni kwamba, wanafunzi ambao walipata daraja la kwanza na pili pekee katika mtihani wa taifa wote walijiunga kidato cha tano kwa ufaulu wa daraja la tatu na katika ufaulu wa masomo yao ukiwa wa chini kabisa. Lakini wote walimaliza kwa ufaulu wa daraja la kwanza na pili pekee (hakuna shule yoyote Tanzania iliweza kuweka rekodi hii isipokuwa ni Coastal sekondari pekee). Shule ya sekondai Coastal, iliimarisha mifumo ya ulinzi na usalama wake kwa kuboresha uzio mkubwa wa Ukuta kuzunguka shule yote kwa asilimia 100, imefunga mifumo ya CCTV camera za kisasa katika maeneo yote nyeti ya shule na imeajili walinzi wazoefu kazini na zaidi inafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na kituo kikuu cha Polisi Chumbageni. Hivi sasa shule ya Sekondari Coastal inajivunia mafanikio makubwa kwasababu ndio shule inayoongoza kwa taaluma bora, nidhamu na usalama wa shule na wanafunzi kwa ujumla.
Mission
To ensure that the Education we offer prepares the Boys and Girls in Good Conduct to be accepted in Society and Enable them to join all Level of Higher Education and Being Independent and Patriotic Citizens of the Nation.
Vision
To Provide Quality Education for Tanzanian Boys and Girls, Develop them intellectually, morally and spiritually to be a Good Force in any Society they Live in.
Our School Prayer
Our Almighty and eternal God, the most Gracious, The Most Merciful; may your name be kept holy, let your will be done, forgive us our sin and save us from the fall, your goodness and strength is beyond our reach, give us the courage to stand before your truth, for yours is the Kingdom, the power, and the glory forever. Amen.